Moja ya makala zilizopita
niliwahi kuongelea namna ya kupata mtoto wa kiume na jinsi ya kujua siku za
mwanamke za hatari za kubeba mimba ni zipi lakini watu wengi wamekua
wakinipigia simu kwamba hawakuelewa.
Leo ntarudia maada hii na naomba
msomaji usome kwa makini sana.
Siku za hatari za mwanamke ni
zipi?
Hizi ni siku ambazo mwanamke
akishiriki ngono bila kutumia kinga anapata ujauzito bila wasiwasi wowote labda
kama ana matatizo yanayomfanya asibebe mimba au mwanaume wake ana matatizo.
Utazijuaje siku hizo?
Kwanza kabisa ili ujue siku zako
za hatari lazima ujue idadi ya siku za mzunguko wako. Kuna aina tatu za mzunguko..
mzunguko mrefu ambao unachukua siku 35, mzunguko mfupi unaochukua siku 25 na
ule wa kawaida unaochukua siku 28 na ndio mzunguko ambao watu wengi wanao.
Unajuaje mzunguko wako?
Hesabu siku tangu siku ile ya
kwanza uliyoona siku zako za hedhi mpaka siku moja kabla ya kuona siku zako za
hedhi zinazofuata. Unashauriwa uchukue miezi mitatu mpaka sita ukihesabu ili ue na uhakika
kwamba mzunguko wa tarehe zako haubadiliki, kama umeshahesabu siku za nyuma kabla
ya kusoma makala hii ni vizuri pia. Mfano umeanza kuona siku zako tarehe moja
mwezi wa nne alafu ziko zako zingine ukaziona tarehe 29 mwezi wa nne, chukua 29
toa 1 utapata 28.. maana yake wewe unamzunguko wa siku 28.
Je siku za hatari ni zipi?
siku ya hatari ni siku ya 14 kabla ya kuona hedhi inayofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita na hapa ndio watu wengi wanachanganya na kupata mimba.
http://fettydajohnson.blogspot.com/2015/09/18-only-sex-positionsstaili-zaidi-ya.html
siku ya hatari ni siku ya 14 kabla ya kuona hedhi inayofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita na hapa ndio watu wengi wanachanganya na kupata mimba.
http://fettydajohnson.blogspot.com/2015/09/18-only-sex-positionsstaili-zaidi-ya.html
Mfano kama mzunguko wako ni siku wa kawaida siku 28, chukua 28 toa 14 utapata 14. Hivyo siku
yako ya hatari ni siku ya 14, lakini kwa kua mbegu ya kiume inaweza
kuishi mpaka siku tano na yai la kike linaweza kuishi mpaka masaa 24 ndani ya mfuko wa uzazi basi siku
nne kabla na siku moja baada ya siku ya 14 ni hatari hivyo siku za hatari ni ni siku ya
10,11,12,13,14 na 15.
Kama mzunguko wako ni mrefu labda siku 36 basi chukua 36 toa 14
utapata 22. Hivyo siku ya 22 ni hatari na zingine ni 18,19,20,21,22 na 23.
Kama mzunguko wako ni mfupi, mfano mzunguko wa siku 21, sasa ukichukua
21 ukatoa 14 unapata 7 yaani siku ya saba ni hatari kwa huyu mtu.hivyo siku zingine za hatari ni 3,4,5,6,7[mtoto wa kiume] na 8.
http://fettydajohnson.blogspot.com/2015/09/18-only-sex-positionsstaili-zaidi-ya.html
Dalili kwamba uko kwenye siku za
hatari ni zipi?
Kuongezeka kwa joto kidogo, tumbo
kuuma kidogo, na ute mweupe kutoka sehemu za siri..
mwisho: maelezo hayo hapo juu
yanaweza kusaidia kupanga uzazi, kuchagua jinsia ya mtoto au kutafuta
mtoto. Lakini pia tarehe zote nilizoweka mabano ambazo ndio tarehe yai
linashuka ndio za mtoto wa kiume zingine zote zilizobaki ni za watoto
wa kike.
Post a Comment