Muigizaji wa filamu Shamsa Ford
amefunguka na kusema kwamba tangu aachane na Ex boyfriend wake Dickson
Matoke aliwahi kuwatishia kuwauwa yeye na mwanae zaidi ya mara 10.
Akizungumza alisema…’Ni
kweli wakati nilipokuwa katika mahusiano naye alikuwa ni mtu amb
aye
anapenda sana kuniambia neno nitakuuwa mimi na mwanangu ndio maana
nilikuwa naogopa sana kwasababu nilihisi kuwa anaweza kufanya lolote
kunikomoa na nilienda hadi polisi kuchukua RB yake ili kama lolote
litakalotokea basi yeye atakuwa amehusika, yaani yule alikuwa ananiambia
kabia yuko serious mbaya kuwa ataniuwa mimi na mtoto wangu lisha kwangu
alikuwa anawaambia hata marafiki zangu ni mashahidi na mbaya zaidi
alikuwa anasema hayo maneno na mbaya zaidi alikuwa anawaambia hata ndugu
zake.Hayo maneno alikuwa anayaongea wakati bado niko naye kwenye uhusiano lakini ndio hivyo malumbano malumbano na mimi nilikuwa nimeshachoka na hizo tabia zake lakini baada ya kuachana naye ni vitisho labda anataka kumuona mtoto anatumia vitisho mara sasa ninapomnyima mtoto basi anatumia vitisho basi mimi nikikumbuka lile neon lake la kusema ataniuwa basi moyoni sina amani….’alisema.
Post a Comment