Featured
Loading...

SENTENSI 57 ZA DR SLAA ZINAZO MKOSESHA RAHA LOWASSA SOMA HAPA NI HATARI,Nilimwambia LOWASSA wewe na wenzako ni mafisadi kichwani




1. Katika maisha yangu yote sijawahi kuona waandishi wengi hivi, ni dalili kwamba watu wanakiu ya kujua
2. Ningependa nianze kwamba niliamua kufanya kazi hii leo kwa sababu inafika mahali ukweli lazima usemwe
3. Wengi mnafahamu kwamba sina tabia ya kuyumbishwa na ninasimamia kile ambacho ninakiamini mimi
4. Niseme tu pia sina chuki na mtu yoyote wala kiongozi yoyote wa chama chochote ingawa nimesikia mengi
5. Mimi sikuwa likizo kama mlivyoambiwa na wengine, kuna mambo ambayo yalinifanya niwe kimya kwa muda
6. Niliamua kuachana na siasa baada ya kuona mambo hayaendi sawa kama nilivyotegemea ndani ya chama changu
7. Baada ya LOWASSA kutajwa, mpambe wake Askofu GWAJIMA alinipigia simu akiniambia Dodoma mambo yameiva
8. Kama utaratibu, LOWASSA baada ya kusema anahama CCM, alipaswa ajisafishe na tuhuma zote alizokuwa nazo
9. LOWASSA hakufanya hivyo, alipaswa kufanya hivyo akiwa peke yake na si viongozi wa chama anachokwenda
10. Si kwamba nilikuwa sitaki LOWASSA agombee Urais,nilitaka tupate mgombea mwenye sifa zote zinazotakiwa
11. Mimi sikuwa na shida ya kugombea Urais, ningekuwa nataka ningechukua fomu siku ya kwanza walipotangaza
12. Wakati hayo yanaendelea nilikuwa nasimamia uteuzi wa viongozi mbalimbali ndani ya CHADEMA
13. Sikuambiwa lolote kama LOWASSA ni Asset au liability ndani ya Chama chetu na ndio maana nilikuwa sielewi
14. Niliandika barua ya kujiuzulu lakini Prof SAFARI akaichana, sikukata tamaa nikaandika tena
15. Niliandika tena taarifa rasmi kupeleka kwenye chama,hawajui ukitaka kujiuzulu haina hata haja ya kueleza
16. Maneno mengi yalisemwa mara nimefungiwa ndani na mke wangu, mara nitaitisha kikao na waandishi kesho
17. Walisema Dk Slaa analipwa milioni 7 na CHADEMA,napenda kusema familia yangu inaishi maisha ya kawaida
18. Mimi na SUMAYE tunagombana kila siku kwa kuchukua shamba kubwa pale Kibaigwa, alafu leo anajiita msafi
19. Niliahidi mwaka huu CHADEMA hatuchukui Makapi, lakini naona wote waliokuja ni mizigo, nawajua A mpaka Z
20. Ndio maana mpaka leo viongozi wangu wamebaki vigugumizi ndio maana mpaka leo hawawezi kusema lolote
21. Leo LOWASSA anasimama jukwaani na kusema leteni ushahidi wa ufisadi hata bado hajapewa kadi ya chama
22. CCM wamekuwa waoga kutoa ushahidi wa mafisadi, na hata LOWASSA alipofikia ni CCM imemlea
23. Mwaka 2008 Nilikuwa bungeni kuzungumzia Richmond, tuliyajadili Bungeni wote,hatukuyasoma magazetini
24. Mimi ninamlaumu LOWASSA kwa mambo mengi sana na si kashfa ya Richmond pekee kama watu wanavyofikiria
25. Ni bora nipotee kwenye siasa kabisa kuliko kukumbatia mambo maovu kama haya yanayoendelea sasa
26. Ni bora nipotee kwenye siasa kabisa kuliko kukumbatia mambo maovu kama haya yanayoendelea sasa
27. Mimi nimeletewa rushwa hadharani asubuhi, nikamwambia kama unanipa milioni 500 nyingine unazitoa wapi?
28. Milioni 500 ni nyingi sana, Rushwa ni kitu kinachoanzia kichwani na si katika mazingira ya kawaida
29. Mnaweza kusema kwa nini namsema LOWASSA tu, mkumbuke anagombea Urais wa nchi, ukweli hawezi kuvumilika
30. Nilimwambia LOWASSA wewe na wenzako ni mafisadi kichwani, kwenye nafsi na moyoni alafu nikakimbia
31. Nimemsikia MWAKYEMBE na SITTA wanamuomba LOWASSA kwenye mjadala ili aweze kueleza mambo yake, safii
32. Naumia sana kuona CHADEMA yangu niliyotoka nayo mbali na kufika hapa leo inafikia hatua haiaminiki tena
33. Sehemu kubwa ya hotuba ya Jangwani ni ilani yetu ambayo tulishaandika toka zamani,LOWASSA hakuweka kipya
34. LOWASSA achunguzwe zaidi ya Paundi milioni 400 alizopeleka Marekani, wanaomtetea watoke hadharani wakitaka
35. Vijana wengi wakisikia CHADEMA wanashawishika, lakini napenda kuwaambia baadaye tusije kulaumiana
36. Mimi huwa naongea kwa kujiamini sana, na siwezi kwenda kushtaki mahakamani, anayetaka kwenda aende
37. Mimi sitaki kuingilia sana mambo ya Kina Babu Seya lakini naomba wanasheria wetu wajitokeze kusema
38. Akili ya LOWASSA ipimwe,kesi ya ulawiti Rais hapaswi kuingilia, anaingilia uhuru wa mahakama
39. Afadhali kutokuwa na Rais kama huyo,ni Rais balaa ambaye hawezi kuthamini maisha ya Watanzania
40. Akiwa Waziri mkuu alibadilisha hata mpaka wa Monduli na Karatu ambapo mgogoro upo mpaka sasa
41. Nimestaafu siasa ina maana sina Chama lakini haimaanishi sina nchi, nitabaki kuwa mtetezi wa wanyonge
42. Nimeombwa kugombea Urais karibu vyama vitano nimekataa kwa kuwa siamini wala sitaki kuyumbishwa
43. Najua hela za ROSTAM AZIZ ndio zinasaidia mambo ya uchaguzi, pesa zinagawanya kila kona ya nchi
44. Hakuna kipindi nimepata vitisho kama hiki, hata kipindi cha kutaja List of shame haikuwa hivi
45. Kama kuna Maaskofu mmehongwa nchi hii ni bora mkaenda mbele za Mungu kutubu na kuomba msamaha
46. Narudia tena siendi wala sitakwenda chama kingine chochote nitakuwa Mtanzania wa kawaida kama wengine
47. Namtaka LOWASSA leo atoke hadharani atuambie Richmond ni ya Nani? na huyo mkubwa ni nani? si kazi rahisi
48. Nataka ripoti ya Richmond iwekwe hadharani ili wale wanaopiga propaganda waadhirike ili watu wawaelewe
49. Sina sababu ya kurudisha kadi, ni sawa na kadi ya ndoa,ni mali yangu, ni kumbukumbu katika maisha yangu
50. Sina ugomvi na MBOWE ni vyema nikasema, hata nyumba ninayoishi alinisaidia, itakuaje niwe na chuki naye
51. CCM wanilitaka niachie jimbo la Karatu mwaka 2000, nikawaambia sharti saini 3, ya Rais, yangu na ya YESU
52. Nilimshukuru Mungu kutokwenda CCM kwa sababu ningefukuzwa ndani ya miezi mitatu kwa kuwa nisingekubali
53. Simpigii kampeni mtu yoyote lakini nimefanya utafiti kuona Taifa litapata hasara gani akichaguliwa LOWASSA
54. Niliambiwa nina dk5 za kuishi, piga magoti muombe Mungu wako akusaidie baada ya kutaja ufisadi wao
55. Kuhama chama ni jambo la kawaida katika siasa, tatizo anayehama chama huko alipokuwa awali alikuwaje?
56. Kuhama chama ni jambo la kawaida katika siasa, tatizo anayehama chama huko alipokuwa awali alikuwaje?
57. Silaha huziweki zote mezani, nimewaomba wahusika wajitokeze, wakifanya hivyo nitarudi tena kuzungumza

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright Swahili News | Designed By Code Nirvana
Back To Top